Ombi la kila siku
Roho Mtakatifu nijaze!
Omba Roho Mtakatifu afanye kazi ndani yako na akutumie.
Yesu nilinde!
Jiweke katika ulinzi wa Dhabihu na damu ya Yesu.
Baba wa mbinguni, nibariki na unipe nitakayoitaji leo.
Mungu anaweza kupa yote unayohitaji leo.
Ahsante, kwa uhai wangu na yo unayonipa.
Sema shukrani wakati wowote na kwa lolote.
Vaa silaha zote za Mungu
- Chapeo ya Wokovu: Mungu, linda na ubadilishe mawazo yangu.
- Dirii ya Haki kifuani: Ahsante, Mungu, kwa neema uliyoniokoa.
- Ukweli kama Ukanda kiunoni: Mungu, nisaidie niongee ukweli na niishi kulingana na ukweli wako.
- Viatu vya Hamu na Utayari: Mungu, nisaidie kuona nyakati ambazo naweza kueleza kukuhusu na unipe ujasiri kutenda vilivyo.
- Ngao ya Imani: Mungu ninakuamini. Ninaomba imani yangu kwako iendelee kukua.
- Upanga / Neno la Mungu: Mungu, nisaidie kuelewa neno lako na kulitumia.
(Waefeso 6:10-17)